Header Ads Widget

Injili Vs Maadili.


 INJILI vs MAADILI

1. Injili inamwambia Mtu kuwa tatizo la Dhambi na mauti limetatuliwa na Mtu aitwae Kristo Yesu. 


Ya kwamba Yesu alisulubiwa, alikufa, akazikwa na kufuka kwa ajili ya dhambi zetu. Na kwamba kila amwaminiye anapata msamaha wa dhambi, anatakaswa na kupata uzima wa milele. 


2. Na kwamba anatolewa kwenye kifungo cha dhambi, asiwe mtumwa wa dhambi tena. Yaani Mwili wa dhambi unasulubiwa pamoja na Yesu, ili mwili wa dhambi ubatilike asiwe mtumwa wa dhambi tena. 


Asema "mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;" (warumi 6:6)


SASA MPOTOFU NI ANAYESISITIZA MSAMAHA WA DHAMBI BILA KUONESHA USHINDI (neema) DHIDI YA DHAMBI KWA KILA AAMINIYE. 


INJILI INAYOSISITIZA MSAMAHA WA DHAMBI PASIPO UKOMBOZI KWENYE UTUMWA WA DHAMBI NI INJILI BANDIA, HIYO SIO INJILI YA MUNGU AMBAYO NI NGUVU ILITAYO WOKOVU (wokovu kutoka katika mauti na dhambi). 


Ukijumlisha Namba 1 + 2 ndio tunasema huyu katakaswa. (kawa safi kwa damu ya Yesu/mwili wake, na katengwa kutoka kwenye duniani na vitu vyake kwa njia ya kusulubisha mwili na kuunganika katika mauti ya Yesu). 


Yaani anatolewa kwenye utumwa wa dhambi na mauti. dhambi haiwi Bosi wake tena. 


1. Msamaha wa Dhambi ulio katika imani Ya Kristo Yesu 

2. Uhuru kutoka kwenye utumwa wa dhambi na mwili wa dhambi, kutoka katika Kulubiwa kwake Kristo Yesu.


HAYA👆 MAWILI NI INJILI MOJA, PANDE MBILI ZA SHILINGI MOJA.  HUWEZI KUTENGANISHA. 


Hivyo huwezi kusema unahubiri injili kama injili hiyo haizai tunda la Kazi ya msalaba yaani kusulubiwa kwa mwili wa aaminiye na kufa pamoja na Kristo. 


Warumi 6:3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.


HIVYO BASI;


1. INAKUWA HALALI KUMWAMBIA MTU WA YESU "IKIMBIE ZINAA" kwakuwa tayari mwili wa zinaa umeshasulubiwa na kubatilishwa. hivyo anao uwezo wa "KUIKIMBIA ZINAA" kwakuwa dhambi soi bosi wake tena.


Hivyo ukiwaambia wakristo wasiwe waovu au waache uovu hapo hauhubiri maadili bali unahibiri injili na kuitetea na kutaka watu wazae matunda sawasawa na kazi ya msallaba iliyotendeka ndani yao.


Matendo 26:20 ... ya kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Hivyo asema 👇


1KOR 5:11 naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu[ANAJIITA MKRISTO], akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.


HUYO👆 ANAJIITA "MKRISTO" LAKINI HAKUNA ISHARA YA KUONESHA KAZI YA MSALABA IMETENDEKA NDANI YAKE. 

 

KWANINI  ? 👇


Kwasababu "hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake "(gal 5:24)


2. Inakuwa halali kumwambia "mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli" (Waefeso 4:24) 


3. Inakuwa halali kumwambia Mkristo ASIVAE NA KUENENDA KIZINAA na KIKAHABA KAMA WATU WA DUNIA HII, WALA ASIIPENDE DUNIA, KWAKUWA DUNIA IMESULUBIWA KWAKE. 


1Yoh 2: 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.


KWANINI ANASEMA HIVYO👆 ?  KWASABABU 👇


Gal 5: 14 ...  msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.


Hitimisho👇


HIVYO UKIONA MTU ANAWAAMBIA WAKRISTO WASIFANYE MAOVU USIDHANI ANAHUBIRI MAADILI bali anahubiri injili kwakuwa injili ndiyo inakufanya uwe na maadili na uzima, INJILI YA YESU NDIYO HUO UZIMA WENYE HAYO MAADILI YAKE.


hakuna injili ya Yesu unayokupa Uzima bila maadili. HAKUNA. HIYO NI INJILI BANDIA AMBAYO SIO NGUVU ZA MUNGU ZILETAZO WOKOVU (UZIMA WA MILELE NA UHURU KUTOKA KATIKA UTUMWA WA DHAMBI). 


Hivyo hakuna mtu atasema "namwamini Yesu:" Halafu akabaki kuwa mwabudu sanamu na mzinzi na mchawi. HAIWEZEKANI. 


___________

Ibrahim Nzunda 

0754210627

.

Post a Comment

0 Comments