Header Ads Widget

Jinsi ya kugeuza Makosa yako kua Darasa la wewe kutimiza ndoto zako.


 Kama uliwahi kukosea soma hapa


NA EV MAGRETH CHILINGO SEMBUCHE


 Jifunze kusema na moyo wako, nakuuambia  moyo wako, ni kweli uliwahi kukosea, lakini hayo makosa uliyowahi kukosea, yasisabibashe ushindwe  kuendelea, kwa sababu ya makosa uliyowahi kufanya,  mbele ya hayo makosa kuna kitu ambacho ni bora ukiyafanya yawe darasa.


 Na Mungu alivyo sio yeye ambae huwa anaeshuka duniani kukuletea vile unavyotaka kuwa.Ni wewe mwenyewe ndo unaamua,  usijimalize kwa kutokujisamehe.


Kumbuka ukijisamehe kila kitu kitakuwa sawa, maana Mungu amekupa  kuamua, mauti na uzima vipo katika midomo yako  ukiamua kuendelea uta enjoy maisha, na ukaamua kujitesa na kuamua kujiuwa ni wewe mwenyewe. 


Kuna hawa watu wawili waliwahi kufanya kosa moja, Yuda na Petro walifanya dhambi moja  walimsaliti Yesu, tena Petro  alimsaliti mara tatu  na Yuda mara moja. Ila Yuda alijinyonga kwa makosa. Lakini Petro alisema hapana bado nina nafasi ya kutubu na Yesu akamwambia Petro, shetani amekusudia kuwapepeta ninyi kama ngano.


Kwa hiyo kumbe kila mtu ana pepeto lake, wengine pepeto  lao ni kazini kwao, wengine wazazi, wengine kwenye huduma, lakini hata wapendwa wenzio wanaweza kukupepeta,na wengine maisha.


 Ila Yesu anasema hivi nimekuombea, kumbe kila mtu ana neema yakuombewa na Yesu ila pepeto lipo, halafu anasema nikiisha kuwaombea uwaimalishe na wengine, wape  kujiona wapo huru.


 Mungu Mungu akupe Neema yakuwaonyesha watu kwamba wanaweza kutoka kwenye mashimo,    na kwenye majuto, jitoe kwenye kujihukumu upokee uzima, kwani hukumu inaleta mauti bali msamaha unaleta uzima.


 Maamuzi yasiyo faa yamekugharimu bali ndani ya neno kuna uzima.Na usisahau hili unapopita geti la Farao usisahau kuna geti la bahari ya Shamu. usipambane na adui, angalia neema iliyopo mbele yako.


  Usigombane na shetani kwa sababu  ana lebo ya ahetani, Yesu hakugombana na shetani kila mahali, aliangalia  mahusiano yake na Mungu  na mapenzi ya Mungu kwake.


 Mungu akikwambia hiki kitu nicha kwako hata kama wamejipanga watu wengi namna gani, hata kama mazingira yanakatae vipi, hata kama wanadamu wapinge vipi,  wawe na nguvu kuliko wewe, wawe na fedha kuliwe wewe, yafaa uwe na uelewa na ufahamu kukipata kile Mungu amesema juu yako sio wanadamu wanasema juu yako.


  Mungu anaweza kukufikia na baraka ya Mungu inaweza kukufikia lakini kana hauna ufahamu  au uelewa,  huwezi kuwa mshiriki wa hiyo baraka, maana maandiko yanasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.


 Kumbe baraka inaweza ikaja kabisa kukuokoa lakini kama hauna maarifa ya ile baraka unaangamia na baraka unayo.


 Ndio maana unaweza ukawa una silaha lakini umiliki wa silaha haukufanyi wewe uondoke  kwenye hatari kama hujui kuitumia, baraka ya Bwana haijachangamani na majuto, nikwa namna gani hiyo baraka ya Bwana ina tajirisha na baraka ya Mungu sio hela, sio nyumba, ila baraka ya Mungu inaleta vyote hivyo, baraka ya Mungu uwepo wake unavuta hivi vingine, maana baraka ni nguvu ya Mungu kwenye maisha ya mtu, kumletea mema sio kumtendea elewa hapo kuna tofauti ya kukutendea nakukutea.


         Sema amen kama unayo amani.



*EV MAGRETH CHILINGO SEMBUCHE 0672883086*


*magrethsembuche@gmai*

            Waweza wasiliana na Mwandishi moja kwa moja pia karibu kwa maoni yako hapa chini.

Post a Comment

0 Comments