✍🏻Kumekua na maswali mengi sana kwa watu wakitaka kujua jinsi ya kuanzisha Kituo cha Redio mtandaoni, na wengine wamekua wakikurupuka kuanzisha vituo bila kupata maelekezo kamili na mwisho huishia njiani na kutelekeza wazo hilo.
✍🏻Eku Fm imekua ni msaada kwa wengi wanaotaka kufanya vema katika soko la redio mtandaoni, tangu kuanzishwa kwa Eku Fm kumeibua vijana wengi wenye shauku ya kuendesha vituo vyao vya redio mtandaoni na kupitia darasa letu maalum la Eku fm limefanikiwa kuwafikia vijana wengi na wao kufanikisha kumiliki vituo vyao.
✍🏻Eku Fm ni kituo bora kabisa cha redio mtandaoni kilichokusudia kutatua changamoto za ajira kwa vijana kwa kutoa hamasa za elimu ya kujiajiri, namna bora ya kufungua Kituo cha Redio na jinsi ya kukiendesha kwa faida .
✍🏻Katika mada hii leo tutangaalia vipengele vichache vya kutusaidia na kisha wewe unaependa kujifunza zaidi utaendelea kufuatilia mafunzo hapa hapa.
🤔Tuanze na swali je inagharimu kiasi gani kufungua kituo cha redio?
Kuanza safari ya kuanzisha kituo cha redio ya mtandao (internet Radio) inahusisha uwekezaji wa kimkakati katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na vifaa, mpangilio(program),leseni, na gharama zinazoendelea za uendeshaji. Kwa kupata ufahamu wa kina unaweza kupanga na kutenga bajeti yako vizuri ili kuunda kituo kinachostawi. Ili upate ufahamu wa kina usisite kuwasiliana nasi tukupe darasa maalum.
✍🏻Uwekezaji wa awali ni kati ya $1000 hadi 1500 kwa wale wanaoanza msingi, bajeti hii inajumuisha vitu muhimu kama vile maikrofoni, Kichanganyi yaani (sound card ) na Kompyuta.
Ukitaka usanidi wa kitaalam yaani kituo kikubwa unapaswa kutarajia kuwekeza kati ya $3000 na $5000,ikijumuisha vifaa vya kiwango cha juu na leseni ya kina itakayo kupa wigo mpana wa biashara yako.
✍🏻Hivyo ukisha pata wazo la kumiliki Redio ya mtandao ni lazima uwe na majibu ya kwanini unataka kumiliki kituo cha Redio na unataka kuwafikia watu gani na kwa namna gani, ikiwa hujaelewa usisite kutuuliza juu ya wazo la biashara ya Redio.
Ukisha pata ufahamu wa kina bado waweza anza hata kwa $600 tu kisha ukaanza kujiongeza taratibu mpaka kiwango bora cha kituo chako unachotaka.
✍🏻EKU FM imesaidia kupanua watu wengi fikra zao na kuwashika mkono kuanzia hatua za awali mpaka kusimama vema na hata sasa viko vituo vingi vya Redio ya mtandao vinavyo fanya vizuri kwa msaada na ushauri toka kwa watalamu wetu wa EKU FM.
Baadhi ya Radio hizo ni hizi hapa Chini.
✍🏻Kupitia muongozo na ushauri wa namna njema ya kuanzisha kituo bora cha mtandao redio hizo zimeweza kuanzishwa na zinafanya vema katika soko la mtandao.
✍🏻Lazima ujue namna ya kupanga vema bajeti yako kutokana na ukubwa wa malengo yako juu ya uendeshaji muhimu unaoutaka wa Redio.
✍🏻Uwekezaji wa busara huhakikisha kwamba kituo chako cha redio cha mtandao kinakudhi mahitaji ya watu unaotaka kuwafikia
Tambua kwamba mtandaoni kuna aina zote za hadhira , wapo watoto, wapo vijana na wazee pia ambao wanatumia mtandao , kituo chako cha redio lazima kijipambanue kama kitakua ni cha mziki tu, ama kitakua ni cha dini tu ama kitakua ni cha kutoa elimu kwa jamii haya yote lazima uyafahamu kabla hujaanza mchakato wa kufungua.
✍🏻Kuanzisha kituo cha redio mtandaoni kunahitaji vifaa na programu maalum ili kuhakikisha utangazaji wako ama matangazo yako yanakua na ubora.
✍🏻Hapa tunakupa mwongozo wa kuanzia kwa vifaa bora.
📶Maikrofoni
Maikrofoni ni kiini cha usanidi wako kwa utangazaji ,Maikrofoni kama vile Shure Sm 58 ni bora kwa kupunguza kelele ya chini chini na kuzifanya ziwe bora kwa studio za Nyumbani au mazingira yenye uchezaji mdogo wa acoustic.
✍🏻Ikumbukwe ya kwamba kituo cha redio ya mtandaoni ukishafanya taratibu zote unauwezo wa kuendeshea studio yako nyumbani kwako tu kwa kuanzia si lazima upange ama utafute nyumba kubwa sana ya gharama
✍🏻PC tablet ama Kompyuta ya mezani ama kompyuta ya mkononi.
Hii inategemea katika darasa letu la kupima uwezo wako wa kuendesha maudhui ulifaulu namna gani.
Unaweza anza kurusha maudhui yako kwa simu ya kawaida,Pc tablet ama kompyuta ya mkononi hii yote itatokana na mpango mkakati wako ukoje.
📶Hosting
Hapa ni lazima ujue nani unataka awe host wako katika kuhakikisha kituo chako kinakulipa na kukufanya usikike mbali,kuna host wengi lakin Eku Fm tutakuelez yupi anaefaa kwa kuanzia biashara yako.
✍🏻Ikiwa umeelewa comment hapo chini na ikiwa una swali uliza utapata jibu lako
Na kama unatamani kuingia katika darasa maalum wasiliana nasi kwa namba zetu hapo chini na pia waweza join katika group letu la whats ap.
0 Comments