Header Ads Widget

ZIFAHAMU SIRI ZILIZOFUNGWA KATIKA MANENO


Yawezakana umeweza kuskia makala au vitabu vinaelezea habari za Siri zilizopo katika maneno au yawezakana hujawahi kuskia kabsa juu la jambo Hilo bas usiwe na shaka, Leo kwa jinsi roho wa Mungu alivyo niongoza nitakusaidia kuzifahamu Siri zilizofungwa katika maneno mwisho wa makala hii utakuwa na uwezo wa kutumia maneno yako kufanya vitu vikubwa na kuweza kujua namna ya kuondoka kwenye changamoto. Pia ntaweza kukuonyesha baadhi ya maandiko kutoka kwenye biblia, Kuna msemo unasema " when you know you become free in a certain area" ( kadri unavyojua unakuwa huru kwenye eneo Fulani).


Binadamu alipewa pia uwezo wa kutamka maneno kupitia kinywa chake ili kuweza kuwasiliana wao kwa wao pamoja na viumbe vinavyo wazunguka. Hivyo bas kupitia maneno yatokayo kinywani mwake anaweza akafanya jambo lolote na likawa,, biblia inatwambia twafahamu ulimwengu uliumbwa kwa Imani ambayo ilitokana na maneno ya Mungu kusema vitu na vikawa vinatokea mwanzo 1:1-5

Baada ya kuona utangulizi twende Sasa tukajue je nisiri gani zilizofungwa katika maneno,, tunapo enda kujua hizo Siri jambo kubwa la kufahamu ujue mtu asiye jikwaa katika maneno huyo ni mtu mkamilifu Yakobo 3:2(b)

Huo mstari unaonesha kuwa Kuna Mambo yamefichwa kwenye maneno Sasa usipo weza kujikwaa nayo basi utaweza kusalimika kwenye hayo Mambo ( utakuwa mkamilifu) yaan mwili unaona kabisa unaumwa mtu anakuja kukuliza vipi unaumwa? , ukimjibu ndiyo tayari ushajikwaa au unakili udhaifu.


1. Kwenye maneno Kuna uzima na mauti;

Jambo lolote huwa linaanzia ndani ya moyo wa mwanadam ko Hilo jambo litapata kibari tu baada ya kuwa huyo mtu atakuwa analizungumza Mara kwa Mara na ndiomaana ukiangalia matajiri wengi ukifatikia historia zao walikuwa wanasema Mimi ntakuja kuwa tajiri, ntakujakumiliki kitu fulani ko kadri anavyo kusema kile kitu ndokinapata kibari Cha kutolea, pia ukiwa mtu wa kujiwazia mabaya siku zote basi hayo Mambo lazima yakufike, mtu utashangaa alisema " Mimi itakuwa ninamkosi,nitakuwa nimelogwa au Mimi sjui Kama ntapona, sjui Kama ntafanukiwa" ko hayo maneno hutoa mauti katika mwili wa mtu.ko jifunze kuamka asubuh jitamkie mema ikiwezekana nenda mbele ya kioo anza kujitamkia mazuri utaona faida yake.

2. Kwenye maneno Kuna Baraka na laana.

Usije ukapuuzia mtu yeyote anapokutamkia maneno mabaya kwasababu hicho kitu huwa kinakuwa nikweli kinatokea, biblia inasema "Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo."(Yakobo 3:10).ko mtu akikwambia neno baya usinyamaze kimya mjibu kwa kusema vitu chanya yakatae Yale maneno hasi, pia mtu akikutamkia maneno mazuri usiishie tu kukaa kimya yapokee kwa kusema Amina , mwisho wa siku utakuja kuona matokeo yake,, Kuna maneno wanayozungumzaga walimu shuleni kuwa utafeli wewe yalemaneno huwa yanafanya kazi kweli ko itabidi kuyakataa kwa kusema.

3. Kwenye maneno Kuna ushindi au wokovu.

Biblia inasema "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."(Warumi 10:10). Hii inamaana kwamba Kuna wakati unaweza kutukanwa au kuzungumziwa vibaya au kuchokozwa ili tu uweze kuwajibu watu vibaya ili shetani ajione kakuweza, ko unapo fanyiwa hivyo moyoni mwako unajiona unahaki ya kuwarufishia majibu mabaya lakini ukiamuwa kuwajibu majibu mazuri tofauti na walivyokuwa wakitarajia mwisho utakuwa umeshinda juu ya jaribu Hilo na tayari utakuwa umeokoka, ko naweza kusema kuwa makini Sana nyakati unapo semwa vibaya juu ya majibu unayo waambia watu maana hayo maneno yako ndo yamebeba ushindi.

4.kwenye maneno Kuna utajiri na fedha.

Leo ukiamuwa kutengenezea utajiri na fedha nyingi bas lazima ujifunze na ujue nimaneno gani watu wangependa kuyasikia kwenye jamii ambayo kupitia maneno hayo watu wakiyasikia watakutafuta ili uwasaidie kutatua changamoto zao, kwa mfano mtu yeye anajikita kuzungumzia Mambo ya afya na lishe tu, wengine wanaongelea kilimo ,ufugaji, biashara n.k, ko kulingana na mtu amejikita kuzungumzia maneno ya vitu Fulani bas watu humtafuta kwa gharama zozote zile mwisho hujipatia kipato mfano mzuri ni mwandishi "Nanauka" amekuwa akizungumza maneno ya biashara na utunzajipesa n.k hatimae saiv analipwa pesa nzuri tu. Ko badara ya kupiga umbeya na kusema watu anza kujifunza ni maeneo gani utajikita kuzungumzia jambo Fulani utakuja nishukuru.

5.kwenye maneno Kuna sumu.

Najua umeshamgaa kuona kwenye maneno Kuna sumu inayoweza kuleta mauti, biblia inasema "Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti."(Yakobo 3:8), kutokana na mstari huo hapo utaamini mtu anaweza akakuzuushia maneno ya uongo mwisho ukiruhisu moyo wako kuyaamini bas umekwisha,, ndiomaana ndoa nyingi saiv zinavunjika ni kwasababu ya maneno wanayo ambuwa na marafiki zao, ko hili kuweza kuliepuka hili nikumwita Sana roho mtakatifu ahusike kufanya maamuzi yaliomema maana ukitumia akili za kawaida hauta amua vyema.

Kwenye maneno Kuna roho(spirit).

Ninaposema kwenye maneno Kuna roho ninamaana ya kuwa unapopewa nafasi ya kuzungumza pahara Fulani kuwa makini Sana na maneno unayozungumza Kuna wakati shetani hutuma roho ya uongo ikakae midomoni mwa watu na ndiomaana unaweza ukawa unamwamini Sana mtu Fulani ili akushauri katika Mambo Fulani lakini hiyo siku roho ya uongo ikawa imewekwa kinywani mwake mwisho ukaangukia pabaya.biblia inasema "Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote."(1wafalme 22:20-22) Ko hivyo unaonesha mfalme anausikiliza maneno ya unabii lakin asjue kuwa shetani kaingiza maneno ya uongo vinywani mwa manabii mia nne, ko kwenye maneno Kuna roho ya uongo,roho ya ubora na roho ya hekima niswala tu kumsihi mungu akupe roho njema.

          Jambo la kumalizia;

Unavyo jiona jinsi ulivyo Leo hivyo ni matokeo ya maneno uliotamkiwa na viongonzi wa dini, wazazi, wasalimu na wewe mwenyew,, usje ukasahau kesho yako haijengwi na fedha au Mali ulizo nazo inajengwa na maneno ya kinywa chako.unapoenda mtaani sasaivi nenda huku ukijizungumzia maneno chanya na mungu akakibariki kinywa chako Kama kinywa Cha mungu kinaumba ulimwengu na vitu vijazavyo Dunia bas nakinywa chako kikaumbe Mambo makubwa maishani mwako.

Mungu akubariki na kukufunilia juu ya ulicho kusoma ili usje ukakosa Cha kusema.

#Christian Mwaluseke 

#Afsa manunuzi na ugavi 

#Mtumishi wa mungu.

Contact; +255 672 965 766.

Post a Comment

8 Comments

  1. Asante Mwaluseke kwa ujumbe mzuri je athari ya maneno kwa mtoto inaondokaje anapokua mzima?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana Mr George kwa kusoma makala hii,, athari ya maneno kwa mtoto inaondoka kwa kuyazika maneno aliyotamkiwa akiwa mtoto maneno yote mabaya mfano unasema nazika roho za kufeli,nazika roho za kukataliwa n.k alafu unaanza kupanda maneno mapya ya ushindi, yeremia 1:10(angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.)

      Delete
  2. Shalom Mwalimu Asante sana kwa makala naomba kujua uhalisia wa kuondoa nguvu ya maneno uko katika kutamka ama uko katika Imani?

    ReplyDelete
  3. Asante Sana Mr pastro majula kwakusoma makala hii, nianze nakusema Imani pasipo matendo haiwezi kukusaidia sehemu yoyote utakayo kwenda, ko ilikuondoa nguvu ya maneno inaondolewa na kutamka maneno ya kuondoka Yale maneno mabaya na kutamka maneno mazuri huku ukiwa na Imani kuwa kimeshatokea, mithali 12:15(Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.) bilashaka utakuwa umebarikiwa ko unachokitamka ndo kinatokea hicho hicho

    ReplyDelete
  4. Kuna watu wanajaribu kunitafute eti hawanipati , unaweza nipigia au kutuma ujumbe wasapu namba ni 0672965766,, au 0613118576 au barua pepe mwalusekechristian@gmail.com,, pia kwa NEEMA ya Mungu mwezi huu nitatoa makala nyingine

    ReplyDelete
  5. Asante sana mtumishi nami kwa kuweka ujumbe huu nitakutafuta maana hukua unapatikana.

    ReplyDelete