Header Ads Widget

Usilolijua ni hili.


    Watu wengi  ni waoga wa kufanya mambo makubwa ambayo Mungu ameweka ndani yao, kwa sababu  huwa  kujimilikisha maono ya Mungu aliyoweka ndani yeo na kuyafanya yeo. 


   Siku utakapojua maono si yako,  maono niya Mungu, Hakuna kitu kitakuogopesha kutimiza, maana utajua  sio ya kwako. Nakama sio ya kwako, hautatumia nguvu wala uwezo wako binafsi. Ila aliyekupa , atayawezesha.


  Lakini narudia tena lakini, pamoja na hayo kumbuka uthubutu hausababishwi na Mungu ni wewe ndo Unatakiwa kuthubutu. Nisikie  mtu wa Mungu uthubutu ni wako wewe sio wa Mungu.


 Na usichojua ni hiki watu wengi huwa hawasaport maono, wengi huwa wanasaport matokeo. Ndio maana unatakiwa uwe unafanya tathmini  ya watu wanapokufuata  jiulize kwa nini watu wanakufuata au kukusikiliza, na ukiona watu wanakufuata  kuna matokeo wanapata au kuna kitu wanakifuata 

 fanya kitu ambacho ni nguvu yako kwanza ili hicho kitu kikutambulishe. 


  Na Mungu akikupa nafasi ya ukubwa wowote ule, iwe uongozi, huduma biashara, cheo, au umaarufu, jambo kubwa unalopaswa kuzingatia ni kwamba hauwezi kuwa mkubwa  milele, mbele yako kulikuwa na wakubwa walipita, na nyuma yako kuna wakubwa watarajiwa wanakuja, hivyo hivyo hiyo nafasi ni  ya muda, itendee wema. Maana wadogo wa leo ni wakubwa watarajiwa


Mtego mkubwa ambao lazima uutegue na kuushinda ni wimbo, ambao wadogo  huwa wanaimbiwa. Kuna habari  mbili nitakupa tena zinapatikana kwenye Biblia yako kuhusu Sauli

mkubwa na Daudi  mkubwa mtarajiwa ,soma  maneno haya 1sam 18:7-8


Mkubwa Sauli alishindwa kabisa kuhimili maneno ya wimbo, yaliyosema Sauli kaua maelfu, Daudi kaua makumi elfu, hii hesabu ilimchanganya sana akaadhimia kumuuwa mdogo ili kulinda kiti chake  au nafasi 


Ambacho Sauli hakujua ni hiki, kikawaida mdogo anapata nafasi ya upendeleo, hivyo ikitokea kusifiwa zaidi ni njia ya kumtia moyo maana hajafikia ukubwa bado,,, Hivyo kujaribu kumzimisha ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe.


Kitendo cha Sauli kutaka kumzimisha Daudi, kilikuwa, cha kujidhuru yeye mwenyewe, na kama angejua hili angeshinda wimbo huu wa kukera moyoni mwake, maana badala ya kumzima Daudi Sauli alijizima mwenyewe, wote tunaufahamu mwisho wake.


    Habari ya pili.

Ni ya Yohana Mbatizaji na Yesu Kristo, hawa walifanikiwa kutegua mtego huu, Yohana kama mtangulizi wa Yesu alipopata habari za sifa na mapambio na nyimbo ambazo Yesu anaimbwa mtaani, aliongea maneno ambayo kama Mungu akikupa neema basi yasitoke kwenye moyo wako.  

Soma maneno haya ya mtu aliyeshinda 


 Yoh 3:26

Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.

    Mstari wa 30

Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.


  Swali kwako? 

    Unaposikia habari za  mdogo kufanya makubwa, kwako ni tishio la kufanya ukose usingizi na kutaka kuua kama Sauli? Au furaha yako inatimia kama Yohana?


By

 EV MAGRETH CHILINGO SEMBUCHE 0672883086

Post a Comment

0 Comments