Header Ads Widget

JINSI YA KUPONYA MOYO ULIO UMIA

 

JINSI YA KUPONYA MOYO ULIO UMIA.


SEHEMU YA 4.


WAZAZI WANAWEZA KUUMIZA WATOTO NA WATOTO WANAWEZA KUUMIZA WAZAZI WAO.


1.Wazazi KUUMIZA mioyo ya watoto wao.


 *Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.* 

Wakolosai 3:21


WAZAZI wakiwachokoza watoto wao, watoto wao hukata tamaa kwa maneno mengine watoto wao wataumia.

Kuwachokoza maana yake nini.

i.Kutowapa haki yao

    Haki ya mtoto ni kusomeshwa, kulindwa...nk 

Usipowapa haki yao, utaumiza mioyo yao.

ii.Kuwanyanyasa

iii.Kuwadharirisha

iv.Kuwafanyia vitendo vya kiunyama

Mfano ubakaji, ulawiti...nk

    Kuna wazazi wanabaka na kulawiti watoto wao.. watoto wanaofanyiwa vitendo Kama hivi, huumia moyo.

v.Kutokuwa na muda nao.

Kuna wazazi wako busy na kazi muda wote. Hawana muda na watoto wao. Unawapeleka watoto wako Boarding School, unawaacha muda wote na House made.

     Unaposhindwa kuwa na muda na watoto wako, mioyo ya watoto wako itaumia.

Kutokuwa na muda na watoto wako ni kuwachokoza.


MADHARA YA WATOTO KUUMIZWA NA WAZAZI WAO

i.Kuharibu hatma zao.

Kuna watoto kesho yao inakua mbaya kwa sababu ya wazazi.

Wapo watoto wamelelewa mazingira ya kunyanyaswa na kuumizwa, halafu wanapoteza ujasiri wanakua ni watu wasio jiamini na kesho yao inakua mbaya

ii.Jeraha la moyo wa mtoto linaweza likapona lakini likabaki kovu.

iii.Madhara ya kitabia

Kuna watoto wanakua ni watu wasio ogopa chochote, wapo tayari kwa lolote, watu wa kujitoa muhanga.

Taifa linapokuwa na watoto wengi wa jinsi hii ni hatari sana.


Watoto wa jinsi hii ni matokeo ya makuzi, malezi...nk.


2.Watoto wanaweza KUUMIZA  mioyo ya wazazi wao.


 *Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;  Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.* 

Mithali 10:1


Mtoto mwenye hekima ni yupi?

i.Ni mtoto anaejua wajibu wake.

ii.Mtoto aneheshimu wazazi wake.


Mtoto asiye na hekima huumiza mioyo ya wazazi wake.

Kuwa makini sana. Usiuumize wazazi wako.


Kwanini?


Ukiwaumiza wazazi wako mioyo yao ikiumia wataachilia laana......


Mungu akubariki. Tukutane sehemu ya 5. Wiki ijayo nakaribisha comment zako hapo chini andika unachotamani kutoka katika somo hili.


Mwl.Montana Mpeleta.

WhatsApp &Normal call +255 763 144 769

Email- montanampeleta@gmail.com

Post a Comment

1 Comments

  1. Asante sana kwa somo lako zuri tunaomba uongeze ufafanuzi kidogo

    ReplyDelete