KWANINI "KASONGO" ILITUNGWA.
Jina lake halisi aliitwa Kasongo wa Kanema, alifariki miaka 3 iliyopita na kuzikwa kwenye makaburi ya Lang'ata.....
"Kasongo" imekuwa ikivuma lakini wachache wanajua hadithi ya wimbo huo.
"Kasongo" ilifanywa na bendi ya Super Mazembe, bendi ya Kongo iliyohamia Kenya mwaka wa 1974. wana bendi walikuwa wameenda kumtembelea rafiki yao Kasongo huko Eastleigh, Nairobi.
Walipofika nyumbani kwake, walikutana na mke wa Kasongo na wakamuuliza kama alikuwa nyumbani.
Mke wa Kasongo aliwakaribisha na kuwaambia kwamba alikuwa hajamwona Kasongo kwa siku nyingi na hali yake haikua njema kiuchumi ili kukidhi mahitaji yake hivyo akawaomba rafiki zake wamsaidie kumtafuta mume wake.
zamani, hakukuwa na mtandao na ilikuwa nadra kupata mtu anayemiliki simu. Waliamua kumtumia ujumbe kwa njia ya muziki, wakitumaini kwamba ungemfikia.
wanachama wa Super Mazembe walianza kumtengenezea Kasongo wimbo sebuleni kwake, wakimwambia arudi nyumbani kwa sababu mkewe ana wasiwasi na anamtafuta lakini hampati.
Waliendelea kurekodi wimbo na, kama wanasema, iliyobaki ni historia.
Je nini sasa kimesabibisha wimbo huu ama jina hili kua maarufu upya na wimbo kuonekana kama mpya.
Ni mtumishi mmoja akiwa anafundisha kanisani aliamua kutoa kumbukumbu ya wimbo huo kama mfano wa wanaume wanaotoroka wake zao na kuwaachia majukum ya kulea watoto.Ndipo yule mtumishi akaimba kipande cha wimbo wa Kasongo jinsi marafiki zake walivyokua wakimuita arudi kwa familia yake,sauti ile ya mtumishi yule ilirekodiwa vema na vijana kipande hicho cha wimbo wa kasongo na kurushwa mtandaoni ikawa chanzo cha kutrend upya kwa wimbo huo.
Hii ndio bendi ya Super Mazembe katika mwonekano wao wa uimbaji miaka ile.
Tazama tafsiri sahihi ya wimbo wa Kasongo hapa
Jina la wimbo:
kASONGO -
Waimbaji:
ORCHESTER SUPER MAZEMBE
[Kiitikio]
Kasongo ye yeee, mobali na ngai
[Kasongo mume wangu]
Kasongo nga nawe oo
[Kasongo Ninakufa mwenyewe]
Zonga libala ee
[Rudi kwenye ndoa]
x2
Kasongo yo yo, mobali na ngai
[Kasongo mume wangu]
Kasongo nga nawe oo
[Kasongo ninakufa mkeo]
zonga libala ee
[Rudi kwenye ndoa]
[Kwaya]
Nga na ndako Kasongo
[Nikiwa ndani ya nyumba, Kasongo]
Miso na nzela
[Kukodolea macho barabarani kila wakati]
Soki okozonga dia ee
[Kama utawahi kurudi]
Yebisa nga ye ee
[Nijulishe mpenzi]
[Kwaya]
Libala na ndako Kasongo
[katika aina hii ya ndoa]
Batunaka ngai
[Wako busy kunihoji]
Tata azali wapi ee
[Baba yuko wapi]
Naloba nini ee
[Ninasema nini]
[Kwaya]
[ala]
Chorus X2
Kasongo yo yo, mobali na ngai
[Kasongo mume wangu]
Kasongo nga nawe oo
[Kasongo I am dying]
Zonga libala ee
[Rudi kwenye ndoa]
[kwaya]
Nga na ndako Kasongo
[Akiwa ndani ya nyumba Kasongo]
Miso na nzela
[Kukodolea macho barabarani kila wakati]
Soki okozonga di.
Je kuna jambo zaidi unalijua kuhusu Wimbo huu tuandikie hapo Chini.
0 Comments