MWANADAMU YEYOTE YULE AMEPEWA NGUVU YA UUMBAJI NDANI MWAKE.
Kila unachokitafuta kipo kinywani mwako, maana umepewa nguvu ya uumbaji ndani mwako, lile neno la karibu ndio linafanya yote.
Bwana anafanya kazi siku zote na mwanadamu na sisi tunafanya kazi siku zote, ndio maana kesho yako ina umuhimu sana kuliko dhambi yako, maana dhambi yako ina dawa ina mahali pakwenda, lakini ukipoteza kesho yako, unaweza kwenda mbinguni lakini usiifikie kesho yako aliyo kuandalia Mungu hapa duniani.
Mtu mmoja alikuwa anaitwa Musa hasira ilimzuwia kufika Canaan, yupo mbinguni anakula bata hadi leo, lakini hakuiona kesho yake, Mungu alipokuwa anasema nae alimwambia hawa watu mpaka uwafikishe kwenye nchi niliyo waahidia, kumbuka sio shetani alie mzuwia Musa kufika nchi ya ahadi ni Mungu na akamwambia njoo kwenye mlima Nebo njoo nikuonyeshe nchi ambayo nilikwambia utaenda huendi: akamuonyesha.
Musa alitamani sana na akaomba sana Mungu akakataa,
Ndio maana kesho yako haina mbadala ni kesho yako, na kesho yako aliyokuandalia Mungu niya muhimu kuliko shida ya dhambi yako, kwa sababu dhambi yako ina dawa Msalabani, na una mahali pakwenda nayo na ukaitupa huko, lakini ukipoteza kesho yako umepoteza jumla.
Sasa kwa sababu kesho yako niya muhimu sana, jiwekee sheria usibebe msongo wa mtu, watu wengi wanaokuga wanawasumbua watu wanakuwaga na misongo yao na wanatafuta pakupumulia,usibebe mzigo wa mtu hata kama akikutukana. Jizungumzie vizuri binafsi, unapoiendea kesho yako.
Nakuombea sana jitafute ujipate, ujue kitu gani kilichopo ndani yako, achana na roho yakuiga iga kila unaemuona unataka kuwa kama yeye, na ujue nguvu iliyopo ndani yako na ujue kitu gani kilichopo ndani, kumbuka nyakati hazina kazi na watu waliolala, nyakati zina kazi na watu walio amuka.
mwambie jirani yako hiyo nayo ni Injili.
*MAGRETH CHILINGO SEMBUCHE 0672883086*
*magrethsembuche@gmail.com*
0 Comments